Shirika la Msalaba Mwekundu: 40% ya watu nchini Ukraine wanahitaji msaada wa kibinadamu

Shirika la Msabala Mwekundu nchini Ukraine linasema asilimia 40 ya watu nchini humo wanahitaji msaada wa kibinadamu kufuatia uvamizi wa Urusi. Lakini maafisa wamesisitiza ugumu wa kufanya shughuli nchini mwao.

Maafisa wa shirika hilo walihudhuria mkutano mjini Tokyo nchini Japani jana Alhamisi kuelezea hali ya sasa nchini Ukraine kwa wanachama wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Japani.

Walisema wanachama wanane wa shirika hilo la Ukraine waliuawa katika uvamizi huo na ofisi zake 23 kuharibiwa.

Afisa wa Ukraine alielezea matumaini kuwa wanafunzi wataendelea na majadiliano na mazungumzo kuhusu Ukraine kama sehemu ya juhudi zao za kuunga mkono nchi hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Ukraine Maksym Dotsenko alisema kuna hitaji linaloongezeka la kuwasaidia watu nchini humo. Aliongeza kuwa ni muhimu zaidi kudumisha maslahi ya watu nchini Ukraine kwani bado haijabainika ni lini vita vitamalizika.

Mfanyakazi mmoja wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Japani aliyeshiriki mkutano huo alisema shirika hilo litafanya kila liwezalo kuwasaidia watu wenye mahitaji.