Wachambuzi wa Uingereza: Vikosi vya Urusi vinakaribia njia muhimu ya usambazaji mashariki mwa Ukraine

Vikosi vya Urusi vimeendelea kushambulia maeneo lengwa nchini Ukraine jana Jumatano. Mamlaka za Ukraine zimesema raia wawili wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa katika eneo la Kharkiv mashariki mwa Ukraine na Kherson lililopo kusini mwa nchi hiyo.

Katika taarifa yake mpya ya kiintelijensia juzi Jumanne, wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema kwamba kuna uwezekano vikosi vya Urusi vimetwaa udhibiti wa kijiji kilichopo karibu kilomita 20 kaskazini mwa Avdiivka kwenye eneo la mashariki la Donetsk.

Ilisema eneo hilo limeshuhudia mapigano makubwa kipindi chote cha mwaka na Urusi imekuwa ikisogea taratibu tangu ilipoitwaa ngome ya Ukraine ya Avdiivka mwezi Februari.

Wizara hiyo ilisema moja ya njia kuu ya usambazaji kwa vikosi vya Ukraine mashariki zaidi ya kijiji hicho inaweza kukumbwa na tishio la kukatwa na usafiri kutatizika.