Utalii wa Hakone warejea kwa takribani asilimia 90 ya kiwango cha kabla ya janga la korona

Watalii wamerejea katika mji wa kitalii wa Hakone, karibu na Tokyo. Idadi ya wageni iliyopatikana mwaka jana ilikuwa karibu asilimia 90 ya ilivyokuwa kabla ya janga la virusi vya korona.

Maafisa wa eneo hilo wanasema watalii milioni 19.51 walitembelea mji huo wa milimani katika Mkoa wa Kanagawa mwaka 2023. Idadi hiyo ipo juu kwa asilimia 12.4 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Kabla ya janga la virusi vya korona, Hakone ilipokea watalii milioni 21.26 mnamo 2018. Idadi ya mwaka jana ilifikia karibu asilimia 90 ya hiyo.