Manispaa za Japani kuhamasisha uzuri jijini Beijing ili kuvutia watalii kutoka China

Zaidi ya manispaa kumi na mbili zimejinadi zenyewe katika vituo vya utalii jijini Beijing wakati huu wa kasi ndogo ya urejeaji katika hali ya kawaida kwa idadi ya watalii wanaotembelea Japani.

Maafisa walipaza sauti zao katika tukio lililoandaliwa na jiji la Beijing kabla ya msimu wa likizo ya msimu wa joto.

Serikali za maeneo 16 za Japani zilitengeneza mabanda ya maonesho katika tukio hilo, sambamba na manispaa na makampuni nchini China na kwingineko.

Wawakilishi katika banda la Mkoa wa Yamagata walionesha mchezo wa kitamaduni wa Kijapani wa kikombe na mpira unaoitwa kendama wakati wakitoa vitini vinavyotambulisha vivutio vya watalii.

Washiriki kutoka Mkoa wa Okinawa walifanya onesho la muziki kwa kutumia vifaa vya kitamaduni vyenye nyuzi tatu mbele ya skrini inayoonesha mandhari kutoka maeneo mbalimbali ya Okinawa.

Balozi wa Japani nchini China, Kanasugi Kenji, alitembelea eneo hilo jana Jumamosi. Alielezea umuhimu wa watu kutembelea nchi ya mwingine.

Pia aliwatia moyo watu kuimarisha uelewa wa Japani kupitia tajiriba mbalimbali.

Idadi ya watalii wa kigeni inarejea katika hali ya kawaida kwa kasi. Lakini idadi ya watalii hao kutoka China ambayo ilikuwa kubwa zaidi, ilikuwa chini zaidi ya 530,000 katika mwezi Aprili, kwa mujibu wa Taasisi ya Taifa ya Utalii ya Japani.

Idadi hiyo ni zaidi kidogo ya asilimia 70 ya watalii ambayo waliofika nchini Japani katika kipindi kama hicho mwaka 2019, kabla ya janga la virusi vya korona.

Mwanafunzi mhitimu wa kike ambaye alikwenda katika tukio hilo alisema alikua akitazama anime za Japani, kitu ambacho kinamfanya atake kwenda Japani.