Mkutano wa mawaziri wa BRICS unafanyika nchini Urusi

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za mpangokazi wa BRICS ambazo ni Brazil, Urusi, India, China, Afrika Kusini na zinginezo wameanza mkutano wa siku mbili mjini Nizhny Novgorod katikati mwa Urusi.

Huu ni mkutano wa kwanza wa aina hii tangu Iran, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na nchi zingine kujiunga na kundi hilo mwaka huu.

Wakati wa ufunguzi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na mwenyekiti wa mkutano huo Sergey Lavrov alisema kupanuka kwa BRICS ni wazi kunaonyesha uundaji wa utaratibu wa nchi nyingi zenye nguvu duniani.

Washiriki wanatarajiwa kujadili ushirikiano wa kiulinzi na kichumi.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi inasema kuwa, pamoja na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China Wang Yi na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi wanachama, wanatarajia wawakilishi kutoka nchi 20 za Mashariki ya Kati, Asia na Afrika ambazo ni rafiki kwa Urusi kushiriki. Inasisitiza maslahi makubwa ya kundi la BRICS.

Urusi inaonekana inatumia mwanya huo kuongeza uwepo wa mpangokazi wa BRICS na kuimarisha uhusiano na nchi za Global South kukabiliana na nchi za Magharibi.