Modi wa India aapishwa muhula wake wa tatu kama Waziri Mkuu

Narendra Modi ameanza muhula wake wa tatu mfululizo kama waziri mkuu wa India baada ya muungano unaoongozwa na chama chake kushinda viti vingi katika uchaguzi mkuu wa hivi karibuni.

Modi aliapishwa katika makazi ya rais kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, New Delhi jana Jumapili. Ameahidi kuwatendea haki watu wote kwa mujibu wa katiba.

Viti 543 vya baraza la chini la bunge viliwaniwa kwenye uchaguzi huo. 293, au zaidi ya zinazohitajika kwa ushindi, zilikwenda kwa muungano huo unaoongozwa na chama cha Bharatiya Janata cha Modi. Hata hivyo chama chake kimepata pigo na kupata kura chache za kukiwezesha ushindi chenyewe.

Wachambuzi wanasema serikali ya Modi itahitaji kufanya uamuzi wa kisera baada ya kuzingatia nia ya vyama vya maeneo ya kuunda muungano.

Nadhari inaangaliwa iwapo Modi ataweza kuongoza serikali yake kwa uthabiti na kutekeleza hatua za kukabiliana na changamoto nyingi za kiuchumi, ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana na pengo la utajiri.