Waandamanaji wakusanyika mbele ya Ikulu ya Marekani wakidai kusitishwa mapigano haraka huko Gaza

Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika kwenye mji mkuu wa Marekani, Washington, wakidai kusitishwa mara moja kwa mapigano kati ya Israel na kundi la Kiislamu la Hamas kwenye Ukanda wa Gaza.

Waandamanaji walijitokeza kutoka kote nchi Marekani jana Jumamosi ikiwa ni jibizo la miito ya vikundi ya Waarabu wa Marekani, huku mazungumzo ya kufikia kusitishwa mapigano na kuachiliwa kwa mateka yakiwa yamekwama.

Walijaza uwanja mbele ya Ikulu ya Marekani, wakiwa wamebeba mabango yanayosema "Sitisha mauaji ya kimbari" ama “Sitisha usaidizi wa silaha kwa Israel.”

Mwandamanaji mmoja alisema anataka kuona mbinu za umwagaji damu zikimalizika na watoto kutouawa.

Aliongeza kwamba anataka Rais Joe Biden kufanyia kazi kusitishwa kwa mapigano na kuwa Marekani inapaswa kuacha kuisaidia Israel.

Mwandamanaji mwingine alizungumzia maisha ya watu wengi kupotea kila siku kwenye Ukanda wa Gaza.

Alisema hakuna maneno ya kuelezea kiasi gani jambo hili linavyohuzunisha kwamba “mstari mwekundu” ulivukwa miezi minane iliyopita.

Wengi nchini Marekani wanapaza sauti kuiunga mkono Israel. Lakini wakati watu wengi zaidi wakiuawa huko Gaza, Biden na utawala wake, unaoipatia Israel msaada wa kijeshi, unakabiliwa na ongezeko la ukosoaji.

Vita huko Gaza inaweza kuchangia hisia za wapiga kura kutokuwa na furaha ama matumaini katika uchaguzi wa urais mwezi Novemba.