Putin ataja tena uwezekano wa kutumia silaha za nyuklia

Rais Vladimir Putin wa Urusi amezungumza mara kwa mara juu ya uwezekano wa kutumia silaha za nyuklia katika miaka ya hivi karibuni, na amefanya hivyo tena kwenye kongamano la kiuchumi katika jiji la St. Petersburg nchini Urusi.

Putin alikuwa akijibu maswali ya msimamizi wa mkutano huo jana Ijumaa baada ya kutoa hotuba.

Alisema silaha za nyuklia zinaweza kutumika iwapo uhuru na uadilifu wa eneo la Urusi utakuwa chini ya tishio.

Aliongeza kuwa hadhani kwamba tukio kama hilo halikuweza kutokea, lakini haliwezi kubadili sheria ya nyuklia ya nchi hiyo.

Marekani katika siku za hivi karibuni iliipatia Ukraine ruhusa ya kutumia silaha zilizotengenezwa na Marekani kwa ukomo wa mashambulizi katika eneo la Urusi. Katika mkutano jijini St.Petersburg, Putin alisema nchi yake ina haki ya kusambaza silaha za masafa marefu kwa washirika wake ambao ni wapinzani wa nchi za Magharibi.

Katika hotuba yake, Putin alisema Urusi imesalia kuwa sehemu kuu ya biashara duniani, na kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na mataifa rafiki licha ya vizuizi na vikwazo vyote.