Japani imejiunga na mazoezi ya kijeshi ya Marekani yaliyopanuliwa

Vikosi vya Kujihami vya Japani kwa mara ya kwanza vimejiunga na mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka ya Marekani yanayojulikana kama Valiant Shield 24. Yalianza jana Ijumaa katika eneo la Indo-Pasifiki.

Mazoezi hayo makubwa yanafanyika katika eneo lililopanuliwa linaloanzia kwenye eneo la maji nje ya Guam hadi Japani.

Vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na NHK vilipanda ndege ya mizigo kuangalia zoezi linalohusisha manowari inayobeba ndege za kijeshi ya USS Ronald Reagan inayoendeshwa kwa nishati ya nyuklia nje ya pwani ya kusini mwa Japani.

Kamanda wa jeshi la Marekani Gregory Newkirk alisema ushiriki wa Japani unaonyesha kuwa pande hizo mbili "zinakutana mara kwa mara ili kutoa mafunzo ya kiwango cha juu sana."

Kikosi cha anga za juu cha Marekani pia kinashiriki katika mazoezi hayo, ikionekana kukabiliana na ongezeko la ushawishi wa China nje ya angahewa ya Dunia.