Biden: Netanyahu amenisikiliza kuhusu eneo la Rafah

Rais wa Marekani Joe Biden anasema Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu "anasikiliza" maonyo yake juu ya uvamizi wa kijeshi katika eneo la Rafah lililopo kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Biden alitoa maoni hayo katika mahojiano juzi Alhamisi na mwanahabari wa shirika la habari la ABC News, David Muir.

Muir alimuuliza Biden anafikiria nini juu ya Israeli kuendelea mbele na operesheni katika eneo la Rafah licha ya maonyo yake.

Muir pia alirejelea wataalam ambao wanasema Israeli huenda wametumia silaha kutoka Marekani.

Biden alisema anafikiri Netanyahu ananisikiliza kwa sababu wanajeshi wa Israeli hawajavamia eneo lote la Rafah, au kuingia kwenye jiji hilo "kwa nguvu kamili".

Kuhusu mazungumzo ya kusitisha mapigano na kundi la Hamas, Biden alisema Israeli "imekubali makubaliano muhimu yanayoungwa mkono na karibu ulimwengu wote wa Kiarabu."

Netanyahu hajafafanua msimamo wake.

Hamas inasema haitakubaliana na pendekezo la hivi karibuni, au kuachilia mateka, hadi pale Israel itakaposimamisha mapigano daima.