Mkuu wa UN atoa wito wa kupiga marufuku matangazo ya fueli za visukuku, akionya ‘jehanamu ya hali ya hewa’

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, UN Antonio Guterres ameelezea hisia kali ya janga kufuatia ripoti za shirika la hali ya hewa la Umoja wa Mataifa jana Jumatano zinazosema kwamba kiwango cha ongezeko la joto duniani kinaongezeka.

Katika hotuba aliyoitoa jana Jumatano, Guterres ameiomba jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi zaidi ili kudhibiti ongezeko la joto duniani, akitoa wito wa "kutoka kwenye njia kuu ya kuelekea jehanamu ya hali ya hewa."

Alisema, "Sote tunaweza kuleta mabadiliko, kwa kukumbatia teknolojia safi, kupunguza nishati ya mafuta ya visukuku katika maisha yetu wenyewe."

Kwa kuzingatia kwamba serikali nyingi huzuia au kupiga marufuku utangazaji wa bidhaa zinazodhuru afya ya binadamu, mkuu huyo wa UN alihimiza “kila nchi ipige marufuku matangazo kutoka kwa kampuni za fueli za visukuku.”