Toyota, Mazda kusitisha uzalishaji wa aina 5 ya magari

Kampuni mbili kati ya tano za utengenezaji magari za Japani zilizobainisha mwenendo mbaya wakati wa kuteleza uchunguzi wa ndani uliomriwa na serikali, yamesitisha uzaishaji wa aina za magari zilizoathiriwa kuanzia leo Alhamisi.

Toyota, Mazda, Yamaha, Honda na Suzuki yalibainika Jumatatu wiki hii kuwa na vipimo bandia vya utendaji ili kupata idhini ya serikali kwa magari yao.

Kati ao, Toyota na Mazda zimesitisha uzalishaji wa jumla ya aina tano kwa mujibu wa agizo la wizara ya uchukuzi la kusimamisha usafirishaji wao.

Toyota inasimamasha uzalishaji wa magari yake aina ya Yaris Cross na aina zingine mbili kwenye viwanda vyake kwenye mikoa ya Miyagi na Iwate hadi Juni 28.

Mazda inasimamisha uzalishaji wa Mazda 2 na magari mengine kwenye viwanda vyake katika mikoa ya Hiroshima na Yamaguchi.

Wasiwasi unaongezeka juu ya athari zitakazotokana na uzalishaji kusimamishwa kwa uchumi wa ndani na washirika wa kibiashara.