Kiwango cha jumla cha uzazi nchini Japani kimevunja rekodi ya chini mwaka 2023

Takwimu za serikali ya Japani zinaonyesha kwamba kiwango cha uzazi mwaka jana kilishuka chini zaidi tangu uwekaji rekodi uanze mwaka wa 1947. Idadi ya watoto ambao mwanamke anatarajiwa kupata wakati wa maisha yake ilishuka hadi 1.20.

Jana Jumatano Wizara ya afya ilitoa takwimu za makadirio ya idadi ya watu kwa 2023.

Kiwango cha jumla cha uzazi mwaka jana kilikuwa chini kwa alama 0.06 kutoka takwimu ya mwisho ya mwaka uliopita. Pia takwimu hiyo inafanya ushukaji kuwa wa nane mfululizo wa mwaka hadi mwaka.

Kiwango cha jumla cha uzazi kilipungua katika mikoa yote. Tokyo ilichapisha idadi ya chini zaidi ya 0.99.

Idadi ya watoto Wajapani waliozaliwa mwaka jana ilikuwa 727,277. Ilipungua 43,482 kutoka mwaka juzi na ilikuwa ya chini zaidi tangu rekodi za takwimu zianze mnamo mwaka 1899.

Kulikuwa na vifo 1,575,936 mwaka jana. Hii ilikuwa rekodi ya juu.

Idadi ya ndoa ilikuwa 474,717. Idadi hiyo ilipungua kwa 30,213 mwaka hadi mwaka, na kufanya kiwango cha chini zaidi cha baada ya vita nchini Japani.