Kumbukumbu ya waathiriwa wa tukio la Uwanja wa Tiananmen yafanyika jijini Tokyo

Watu jijini Tokyo wamehudhuria kumbukumbu ya wale waliofariki wakati wa ukandamizaji wa China dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia katika Uwanja wa Tiananmen jijini Beijing miaka 35 iliyopita.

Kumbukumbu hiyo iliyofanyika katika Kata ya Chiyoda jijini Tokyo jana Jumatatu usiku. Karibu watu 50 walihudhuria ibada, wakiwemo wanaharakati Wajapani wanaotetea haki za binadamu na wakazi waliozaliwa China na Hong Kong.