Maafisa wa kikosi cha walinzi wa pwani wajadili meli kubwa ya China iliyopewa jina ‘dubwana’

Meli nyingine kubwa ya Kikosi cha Walinzi wa Pwani cha China ilionekana mwezi jana katika bahari ya China Kusini karibu na Ufilipino. Mamlaka nchini Japani na katika nchi zingine zinafuatilia kwa karibu meli hiyo iliyopewa jina “Dubwana.”

Baadhi ya magazeti ya Ufilipino yanaripoti kuwa meli hiyo ni ya “Kikosi cha Walinzi wa Pwani cha China 5901.” Ni ya ukubwa sawa na ile ambayo huonekana mara kwa mara katika Bahari ya China Mashariki.

Mwezi Mei mwaka huu, meli ya “Kikosi cha Walinzi wa Pwani cha China 5901” iliripotiwa kuingia katika ukanda maalum wa kiuchumi wa Ufilipino na kusafiri katika bahari zilizopo jirani na Scarborough Shoal ambayo kimsingi inadhibitiwa na China.

China inaongeza shnikizo kwa kuzirushia meli za Ufilipino mabomba ya maji katika Bahari ya China Kusini.

Washiriki katika mkutano wa usalama wa Asia uliofanyika nchini Singapore walizingumzia hali hiyo.

Mkuu wa jeshi la wanamaji Ronnie Gil Gavan ambaye ni Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Pwani cha Ufilipino alisema wafuatiliaji wa moto hawakusudiwi kuwasha moto bali kuokoa maisha na mali kutokana na moto.

Seguchi Yoshio ambaye ni Makamu wa Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Pwani cha Japani alisema meli za Walinzi wa Pwani lazima zisitumike kama vyombo vya kubadilisha hali ilivyo.