India: Watu wasiopungua 46 wauawa na joto kali

Vyombo vya habari nchini India vinaripoti kuwa joto kali lilisababisha vifo vya watu wasiopungua 46 mwezi uliopita nchini humo.

Mamlaka za hali ya hewa zinasema halijoto wakati wa mchana zilifikia nyuzi 50.5 za Selisiasi Jumanne wiki iliyopita katika jimbo la magharibi la Rajasthan. Halijoto zimezidi nyuzi 45 kwa siku kadhaa katika maeneo mengi nchini humo.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema watu 33 walifariki kwa kile kinachoshukiwa kuwa ugonjwa wa kuzirai kutokana na joto kali wakati wakifanya kazi katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh wakati wa upigaji kura wa mwisho katika uchaguzi mkuu uliofanyika juzi Jumamosi.

Mamlaka za hali ya hewa zinatoa wito kwa watu kuchukua tahadhari zikisema hatari ya ugonjwa wa kuzirai kutokana na joto kali inaongezeka miongoni mwa watu wanaokaa kwa jua kwa muda mredu au wanaofanya kazi ngumu.