Maafisa wa hali ya hewa waonya hali kutokuwa thabiti katika maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Japani

Maafisa wa hali ya hewa wa Japani wanawashauri watu kuchukua tahadhari ya radi, vimbunga na mvua za maeneo, wakati hali ya anga ikibadilika badilika katika maeneo ya mashariki na kaskazini mwa Japani.

Mamlaka ya Hali ya Hewa imesema kutokana na hewa baridi kuvuma katika mwinuko mkubwa na hewa yenye unyevunyevu kuvuma kuelekea kwenye mfumo wa shinikizo la kidogo ambao unaelekea mashariki mwa Bahari ya Japani.

Hali hiyo imesababisha mawingu ya mvua kujitengeneza katika maeneo ya Kanto, Tokai na Hokuriku.

Hali hiyo ya kubadilika badilika inatarajiwa kuendelea hadi kesho Jumatatu katika maeneo ya mashariki na kaskazini mwa Japani.

Maafisa wa hali ya hewa wanawashauri watu kuwa na tahadhari ya radi, vimbunga na pepo kali pamoja na mvua kubwa za mawe za maeneo.

Watu wanashauriwa kuhakikisha usalama wao kwa kujihifadhi katika majengo imara pale panapotokea kiza cha ghafla, upepo wenye baridi kuanza kupuliza na kuna ishara ya mawingu makubwa yanayojitengeneza kukaribia.