Ufuatiliaji wa kitamaduni wa harusi ya maua ya airisi wafanywa upya

Watalii katika bustani ya pembezoni mwa mto katika Mkoa wa Ibaraki walifurahia harusi ya maua ya airisi wakiwa kwenye boti wakati huu wa uchanuaji kamili.

Mji wa Itako, uliopo kaskazini mashariki mwa Tokyo, umezungukwa na maziwa na mito ambapo boti zinazofanya safari zake ziliwahi kuwa usafiri wa kila siku.

Hadi katika miaka ya 1960, ilikuwa ni desturi kwa bibi harusi waliovalia mavazi meupe ya Kijapani ya kimono kuonekana kwenye safu za mashua ya makasia wakielekea kuonana na wapenzi wao.

Utamaduni huo uliofufuliwa umekuwa angalizo kwa Tamsha la Suigo Itako Airisi la kila mwaka.

Wanandoa waliooana hivi karibuni, ama wale wanaopanga kufunga ndoa walituma maombi kwa mji huo kupata nafasi ya kushiriki katika tukio hilo.

Jana Jumamosi, boti iliyowabeba bibi harusi ilianza safari huku watalii wakiangalia kutokea upande wa mto wakimshangilia.

Wanandoa hao waliungana kwenye gati na baadaye kuendelea kutembea kote kwenye bustani ya airisi.

Bibi harusi Miyamoto Michiko alisema ilikuwa ni siku ya furaha kubwa kwake, na kwamba aliweza kuona kutoka kwenye boti kila mtu akimshangilia kutokea pembezoni mwa mto.

Bwana harusi Miyamoto Kensuke alisema kwamba alifurahishwa kwa pongezi zote walizopokea.

Sherehe hizo zinaweza kushuhudiwa Jumatano, Jumamosi na Jumapili hadi Juni 16.