Waziri wa ulinzi wa Japani: Japani kuwa kinara katika eneo la Indo-Pasifiki

Waziri wa ulinzi wa Japani ameuambia mkutano wa usalama wa Asia kuwa nchi yake “inadhamiria kuongoza juhudi za kukuza na kuimarisha hali huru na wazi ya kimataifa kulingana na utawala wa sheria” katika eneo la Indo-Pasifiki.

Kihara Minoru alitoa hotuba hiyo katika Mkutano wa Usalama wa Asia, unaofahamika pia kama Mkutano wa Shangri-La nchini Singapore jana Jumamosi.

Alisema kwamba jumuiya ya kimataifa inashuhudia “mabadiliko ya upande mmoja ya hali kwa nguvu na vitendo kama hivyo katika Bahari ya China Mashariki na ile ya Kusini.

Kihara ni dhahiri alikuwa akiizungumzia shughuli za baharini zinazoongezeka za China katika maeneo hayo.

Aliongeza kuwa, “Amani na uthabiti katika Mlango Bahari wote wa Taiwan pia ni muhimu.”

Kihara alisema kuendeleza amani na uthabiti katika eneo la Indo-Pasifiki ni kwa maslahi ya wote katika jumuiya ya kimataifa.

Alisema Japani itafanya kazi na “mtandao wa mataifa ambayo yanashirikishana lengo hili.”

Waziri huyo alizungumzia kuhusu uamuzi wa kupata kile kinachoitwa uwezo wa kufanya shambulizi la kulipa kisasi na kuelezea kwamba “Japani kuimarisha uwezo wa ulinzi na ushirikiano na washirika wake na mataifa yenye fikra kama hizo haimaanishi kuongeza wasiwasi katika eneo hilo.”

Aliongeza, “Japani inatafuta kuzuia mabadiliko ya hali ya upande mmoja kwa nguvu ili kutengeneza mazingira mazuri ya usalama.”