Japani, Korea Kusini zakubaliana kurejesha mabadilishano ya kiwango cha juu ya maafisa wa ulinzi

Waziri wa Ulinzi wa Japani Kihara Minoru na mwenzake wa Korea Kusini Shin Won-sik wamekubaliana kurejesha mabadilishano baina ya maafisa waandamizi wa ulinzi baada ya kusitishwa kwa miaka sita. Mabadilishano hayo yalisitishwa baada ya tukio la rada mwaka 2018.

Kihara na Shin walikutana jana Ijumaa pembezoni mwa mkutano wa usalama wa Shangri-La nchini Singapore.

Kihara alisema anataka kujadili ushirikiano wa baadaye wa ulinzi, wakati huu ushirikiano wa pande mbili unapoboreshwa kufuatia uongozi wa nchi zote mbili.

Mawaziri hao walithibitisha maudhui ya hatua za usalama zilizoandaliwa na Vikosi vya Kujihami vya Japani, SDF na Jeshi la Majini la Korea Kusini kuzuia kutokea tena kwa tukio la rada.

Katika tukio la mwaka 2018, Japani inasema manowari ya Jeshi la Majini la Korea Kusini ilielekeza rada ya kudhibiti moto kwenye ndege ya doria ya SDF juu ya Bahari ya Japani. Korea Kusini inakanusha madai hayo.

Jana Jumamosi, mawaziri hawakujadili kwa kina suala hilo. Hatua husika hazikulitaja suala hilo, pia. Hata hivyo, waliainisha kwamba katika tukio ambalo upande mmoja utafikiri kuwa vitendo vinavyofanywa na upande mwingine kuwa vinaweka hatari, na kujaribu kuanzisha mawasiliano, upande mwingine unashauriwa kujibu.

Kihara aliwaambia wanahabari kwamba pande zote mbili zinadumisha misimamo yao kuhusiana na tukio hilo, lakini kutokea tena kutasababisha uharibifu usioweza kurekebishwa.

Alisema kwamba kurejesha mabadilishano kutasaidia kuimarisha ushirikiano wa pande mbili na uhusiano wa nchi hizo mbili na Marekani, na kukuza azimio la changamoto za usalama.