Maafisa wa ulinzi kutoka nchi za Asia na za Magharibi kujadili usalama kwenye Majadiliano ya Shangri-La

Maafisa wa ulinzi kutoka nchi za Asia na nchi za Magharibi wanajiandaa kufanya mikutano nchini Singapore leo Ijumaa.

Majadiliano ya Shangri-La yatakayodumu kwa siku tatu yanawaleta pamoja Mawaziri wa Ulinzi Lloyd Austin wa Marekani, Dong Jun wa China na Kihara Minoru wa Japani miongoni mwa maafisa wengine.

Maafisa hao wanatarajiwa kujadili masuala ya usalama barani Asia, ikiwemo Taiwan, Bahari ya China Kusini na Korea Kaskazini. Pia huenda wakabadilishana maoni juu ya hali nchini Ukraine.

Mikutano ya pande mbili itafanyika kati ya maafisa wa ulinzi wa nchi mbalimbali.

Wakuu wa ulinzi wa Marekani na China watakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu mwezi Novemba mwaka 2022. Angalizo ni iwapo mazungumzo ya ana kwa ana yatasababisha kupungua kwa mivutano kwani nchi hizo mbili bado zimetofautiana juu ya Taiwan na Bahari ya China Kusini.