Japani: Makombora ya Korea Kaskazini yaliangukia nje ya EZZ

Wizara ya Ulinzi ya Japani imesema Korea Kaskazini imerusha makombora kadhaa ya balistiki leo Alhamisi asubuhi. Yote yanaaminika kuangukia nje ya Ukanda Maalum wa Kiuchumi wa Japani, EZZ, na hakuna ripoti za madhara kwa meli au ndege.

Wizara hiyo imesema urushaji huo umefanyika majira ya saa 12:13 asubuhi. Walau moja ya makombora hayo limefika umbali wa juu wa karibu kilomita 100 na mwendo wa kilomita zaidi ya 350.

Yote yanaonekana yameangukia katika pwani ya mashariki mwa Rasi ya Korea.

Waziri Mkuu wa Japani Kishida Fumio amesema serikali yake inakusanya taarifa na kufuatilia hali hiyo.

Wakuu wa Majeshi ya Korea Kusin wamesema inaaminika kwamba Korea Kaskazini ilirusha makombora ya balisiki ya masafa mafupi zaidi ya kumi kuelekea Bahari ya Japani.

Ni urushaji wa saba wa makombora ya balisitiki kwa Korea Kaskazini hadi kufikia sasa kwa mwaka huu.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajiandaa kukutana kwa dharura leo Ijumaa ili kujadili mwitikio kwa urushaji wa satelaiti, kwa ombi la Japani, Marekani na Korea Kusini.

Korea Kaskazini imesema inapinga mkutano huo, ikidai urushaji huo ni halali kulingana na haki yake ya kujilinda.