Blinken: Marekani itarekebisha na kubadili kama inahitajika katika matumizi ya silaha, Ukraine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken hajakanusha uwezekano wa kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za Marekani kushambulia maeneo lengwa nchini Urusi.

Kwenye mkutano na wanahabari huko Moldova jana Jumatano Blinken alisema kwamba Marekani haijahamasisha ama kuwezesha mashambulizi nje ya Ukraine, lakini Ukraine inapaswa kufanya uamuzi wake yenyewe juu ya njia bora ya kujilinda kwa ufanisi.

Kumekuwepo na ongezeko la miito miongoni mwa mataifa ya Magharibi kuondoa baadhi ya vikwazo vya matumizi ya silaha zao huku Urusi ikizidisha mashambulizi yake mashariki mwa Ukraine.