Kim akubali kushindwa urushaji wa satelaiti ya uchunguzi wa kijeshi

Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekiri kwa mara ya kwanza kuwa urushwaji wa mara ya nne wa satelaiti ya uchunguzi wa kijeshi kushindikana juzi Jumatatu.

Gazeti la Chama tawala cha Wafanyakazi la Rodong Sinmun, leo Jumatano limeripoti kuwa jana Jumanne Kim alitoa hotuba kwenye shule ya Sayansi ya Ulinzi. Shule hiyo inatengeneza satelaiti za uchunguzi wa kijeshi.

Kim aliripotiwa akigusia kuwa roketi iliyobeba satelaiti ya uchunguzi wa kijeshi ililipuka angani. Alisema mfumo wa kujiharibu yenyewe uliwaka, kutokana na kasoro katika injini ya hatua ya kwanza.

Kim alisema kwamba umiliki wa satelaiti ya uchunguzi wa kijeshi wa nchi hiyo unahalalishika, kwa kuwa taifa hilo lazima lipambane na vitendo vya kichokozi vya jeshi la Marekani.

Korea Kaskazini imetangaza kuwa mwaka huu inapanga kurusha satelaiti tatu za uchunguzi wa kijeshi. Wanasayansi wa nchi hiyo wanatarajiwa kuchunguza sababu za kushindwa na kufikiria kwa makini muda wa urushwaji wa tano.