Ripoti ya UN yaelezea ‘wasiwasi mkubwa’ kuhusiana na kashfa za Johnny & Associates

Kikundi kazi katika Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu kinachoitwa The Working Group on Business and Human Rights kimeelezea wasiwasi mkubwa kuhusiana na tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomhusisha mwanzilishi aliyefariki wa kampuni ya Kijapani ya vipaji iliyokuwa ikifahamika kama Johnny & Associates.

Kikundi kazi hicho kimetoa ripoti kulingana na matokeo ya utafiti wake wa kwanza uliofanywa nchini Japani kati ya mwezi Julai na Agosti mwaka jana. Ripoti hiyo inajumuisha mapendekezo na ushauri kwa serikali na makampuni ya Japani.

Ripoti hiyo inazungumzia kashfa za unyanyasaji wa kingono zinazomhusisha mwanzilishi wa kampuni hiyo marehemu Johnny Kitagawa.

Inasema kikundi kazi “kina wasiwasi mkubwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono unaowahusisha mamia ya watu wenye vipaji waliojiunga na Johnny and Associates.”

Ripoti hiyo pia inagusia kuwa “vyombo vya habari nchini Japani vimehusishwa vikificha kashfa hizo kwa miongo kadhaa.”

Kikundi kazi hicho kinagusia umuhimu wa vyombo vya habari kufikiria kwa makini madhara ya kutohusishwa kwenye haki za binadamu na kutumia uwezo wao wa ushawishi.

Ripoti hiyo inatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi ujao.