Korea Kaskazini yasema jaribio lake la hivi karibuni la kurusha satelaiti lilishindikana

Korea Kaskazini inasema jaribio lake la hivi karibuni la kurusha satelaiti ya upelelezi wa kijeshi lilishindikana jana Jumatatu, baada ya roketi iliyoibeba satelaiti hiyo kulipuka katikati ya anga.

Mamlaka ya Taifa ya Teknolojia ya Anga za Juu ya Korea Kaskazini ilitoa tangazo hilo kupitia chombo cha habari cha serikali cha Korea Central News. Ilisema kwamba baada ya satelaiti hiyo kurushwa kutoka kituo cha urushaji cha Sohae kilichopo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, roketi hiyo ililipuka wakati wa hatua ya kwanza ya kupaa.

Mamlaka hiyo iliongeza kuwa hitimisho la awali lilikuwa kwamba ajali hiyo inaweza ikahusishwa na utegemeaji wa utendakazi wa injini iliyoendelezwa hivi karibuni.

Hili lilikuwa jaribio la nne la Korea Kaskazini kurusha satelaiti ya upelelezi wa kijeshi kufuatia urushaji wake uliofanywa mwezi Novemba mwaka jana.