Rais wa Ukraine atoa wito kwa viongozi wa Marekani na China kuhudhuria katika mkutano wa amani

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ametoa wito kwa viongozi wa Marekani na China kuhudhuria katika mkutano ujao wa kimataifa wa amani, akiwataka wadhihirishe uongozi wao ili kuleta "amani ya kweli."

Zelenskyy anataka kutumia mkutano utakaofanyika Uswizi mwezi ujao kufanikisha mpango wa amani anaoupigania. Anasema zaidi ya nchi 80 zitahudhuria mkutano huo.

Zelenskyy alisema anawaomba viongozi wa dunia ambao wanajitenga na juhudi za kimataifa za mkutano huo.

Aliwataja Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa China Xi Jinping, na kuwataka waonyeshe uongozi wao "katika kuendeleza amani -- amani ya kweli na si tu kusitisha mapigano."

Mada ambazo rais wa Ukraine anataka zijadiliewe katika mkutano huo ni pamoja na kubadilishana wafungwa na Urusi, nishati na usalama wa nyuklia, na kurejeshwa kwa watoto waliopelekwa Urusi.