Makundi ya Kijapani yaandaa mashindano ya boti za dragoni mjini Guangdong

Mashindano ya kitamaduni ya boti za dragoni ya China yalifanyika kusini mwa nchi hiyo kuhamasisha mabadilishano kati ya Japani na China.

Jumla ya waajiriwa 450 wanaohusika na makampuni ya Kijapani na serikali za maeneo walishiriki katika mashindano hayo jana Jumamosi katika jiji la Foshan kwenye Jimbo la Guangdong.

Mbio hizo ziliandaliwa na makundi ya makampuni yanayohusiana na Japani huko Guangdong na Ofisi za Ubalozi mdogo wa Japani.

Kundi la karibu wanachama 20 wote wakiwa wamevalia mavazi ya kung`aa, na boti za muundo wa dragoni walishindana. Makundi hayo yalipiga makasia kwa nguvu zote katika mwendo wa mita 200.

Mshiriki wa mara ya kwanza alisema kwamba ni jambo lenye mantiki kuwa na tukio la kukuza uhusiano bora.

Mshiriki mwingine alisema kuwa ilikuwa vema, na tulipongezana sote baada ya mashindano.

Mmoja wa waandaaji, Tanabe Hisato, anayeongoza Chama cha Wafanyabiashara cha Japani jijini Guangzhou, alisema anataka kuona mbio hizo zikiendelea katika siku zijkazo.

Aliongeza kuwa ni vema kwamba Wajapani na Wachina wanafurahia utamaduni wa kieneo kwa pamoja kwa mabadilishano mema.