Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar alenga kuendelea kujadiliana na China

Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim, aliyepo ziarani nchini Japani, ameashiria kwamba nchi yake itaendelea na majadiliano na China, huku ikiimarisha uhusiano wake na Japani katika nyanja ya usalama wa baharini.

Anwar alitoa maoni hayo kwenye mkutano wake na wanahabari jijini Tokyo nchini Japani jana Ijumaa.

Alirejelea juu ya China kuongeza shughuli za kijeshi kwenye Bahari ya China Kusini.

Alisema kuna tofauti katika maoni ya nchi hizo mbili, lakini haoni uwezekano wa haraka wa mgogoro wowote kutokea.

Aliongeza kuwa Malaysia imechukua msimamo wa kujiiingiza katika majadiliano na China.

Kwa upande wa uhusiano wake na Japani, Anwar alisema nchi yake inataka kuhakikisha ushirikiano katika usalama wa baharini. Lakini alisisitiza kuwa msimamo wa nchi yake ni kutoegemea upande wowote.