Mfumko wa bei nchini Japani waongezeka Aprili lakini kwa kiwango cha chini kuliko Machi

Bei za mlaji nchini Japani zilipanda mwezi Aprili mwaka huu lakini kwa kiwango cha chini kwa mwezi wa pili mfululizo.

Wizara ya Mambo ya Ndani inasema kipimo cha bei ya mlaji, CPI kiliongezeka kwa asilimia 2.2 kutoka mwaka uliotangulia.

Kipimo hicho hakijumuishi bei zinazoyumba za vyakula visivyosindikwa ambazo hubadilika kulingana na hali ya hewa.

Kipimo cha CPI kwa sasa kimekuwa chini ya asilimia tatu kwa miezi minane mfululizo.