Maswali na Majibu : Cha kufanya maji yanapokatika (4)

(4) Kumhudumia mtoto kukiwa na kiasi kidogo cha maji

NHK inajibu maswali kuhusiana na kukabiliana na majanga. Nchini Japani, maji salama ya bomba hupatikana muda wote. Lakini watu hukabiliwa na usumbufu mkubwa pale tetemeko la ardhi ama majanga mengine yanaposababisha kukatika kwa maji. Katika mfululizo huu, tunakupatia taarifa zitakazokusaidia kuchukua hatua kwa utulivu pale maji yanapokatika. Leo hii tunaangazia namna ya kumhudumia mtoto kukiwa na uhaba wkiasi kidogo cha maji.

Wataalamu wanashauri kumwogesha mtoto wako kila siku, kutokana na ngozi yao kuwa na kiwango cha juu cha metaboliki na hivyo, kutoa kiasi kikubwa cha jasho na mafuta. Lakini inapokuwa vigumu kuwaogesha wakati maji yanapokuwa yamekatika, usafishaji wa sehemu ya mwili kwa kutumia sabuni ya chupa yenye povu unaweza kuwa na ufanisi. Kwa kawaida, unahitaji walau lita kumi za maji kumwogesha mtoto. Lakini unaweza kuwaweka safi kwa kutumia kiasi kidogo cha maji unachoweza kupata kutoka kwenye vituo vya usambazaji kwa kuosha makalio yao, kichwa, shingo na uso badala ya mwili wote. Kwanza, mlaze mtoto wako kifudifudi kwenye kitambaa kisichopitisha maji au taulo. Safisha mwili wao kwa maji ya uvuguvugu kabla ya kumuosha taratibu sehemu za juu zilizotajwa za mwili wake kwa kutumia sabuni nyingi. Kisha mfute sabuni kwa maji ya vuguvugu. Hakikisha unampaka krimu ya kuongeza unyevu mara moja baada ya kumkausha mwili kwa kutumia taulo. Hii itawezesha kuzuia magonjwa ya ngozi na vipele.

Pia, unaweza kutumia vikombe vya karatasi kumlisha mwanao bila ya kusababisha hatari za kiafya pale utakapokuwa umeshindwa kusafisha chupa ya mtoto wakati maji yanapokuwa yamekatika. Safisha mikono yako kwa kutumia viua vijidudu na chemsha maji mathalani kwa kutumia stovu inayohamishika. Hamishia kiasi cha maji kwenye sufuria zinazohifadhi joto na kiasi kwenye kikombe, yanapoweza kupoa. Changanya maziwa ya unga ya mtoto na kiasi cha robo tatu ya maji ya moto kwenye kikombe cha karatasi na ongeza maji kutoka kwenye kikombe cha awali, ambayo sasa yanaweza kuwa yamepoa kwa joto la ndani ya nyumba, na changanya. Hakikisha unaandaaa zaidi kidogo ya kawaida kiwango cha maziwa kwani watoto mara kwa mara huyatapika.

Taarifa hii ni sahihi kuanzia Mei 23, 2024.