UNRWA yasema usambazaji wa chakula huko Rafah umesitishwa

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Palestina, au UNRWA, linasema kwamba usambazaji wa chakula kwenye mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah kwa sasa umesitishwa kutokana na uhaba wa misaada na wasiwasi wa kiusalama.

UNRWA ilisema kwenye mtandao wa kijamii juzi Jumanne kuwa kituo chake cha usambazaji na ghala la Shirika la UN la Mpango wa Chakula Duniani mjini Rafah kwa sasa haliwezi kufikiwa kufuatia oparesheni ya kijeshi inayoendelea kwenye maeneo ya mashariki mwa Rafah.

Watu wengi tayari wamelazimika kuikimbia Rafah kuhamia maeneo mengine ya Gaza, lakini vyombo vya habari vya Israel vimelinukuu jeshi hilo likisema kwamba bado kuna raia wanaokadiriwa kati ya 300,000 hadi 400,000 mjini Rafah.