Japani yalenga jitihada za kidiplomasia kuhakikisha amani na uthabiti katika Mlango Bahari wa Taiwan

Serikali ya Japani inakusudia kuendelea na jitihada za kidiplomasia ili kuhakikisha kuna amani na uthabiti katika Mlango Bahari wa Taiwan kufuatia kuapishwa kwa Rais mpya wa Taiwan Lai Ching-te.

Katika hotuba ya kuapishwa kwake jana Jumatatu, Lai alikanusha madai ya China kwamba Taiwan ni sehemu ya China, akisema, Taiwan na China hazipo chini ya kila moja.

Afisa wa serikali ya China aliikosoa hotuba ya Lai, akisema rais huyo mpya alituma ujumbe hatari unaopuuza maoni ya umma, unaoenda kinyume na nyakati, na unaodhoofisha amani na uthabiti katika Mlango Bahari wa Taiwan. Afisa huyo alisema hotuba hiyo iliweka wazi asili ya Lai ya kuwa “mfanyakazi wa uhuru wa Taiwan.”

Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Japani Hayashi Yoshimasa alisema kuhakikisha amani na uthabiti katika Mlango Bahari wa Taiwan ni muhimu kwa jumuiya ya kimataifa, ikiwemo Japani. Hayashi alisema msimamo endelevu wa Japani ni kwamba nchi hiyo inatarajia masuala yanayohusiana na Taiwan kutatuliwa kwa njia ya amani kupitia majadiliano.