Japani kutumia teknolojia ya AI na droni kuondoa mabomu ya ardhini katika mpango wake rasmi wa usaidizi wa maendeleo

Wizara ya mambo ya nje ya Japani inapanga kuanza kutumia teknolojia ya akili kompyuta AI na droni kusaidia kuondoa mabomu yaliyotegwa ardhini katika nchi zinazoendelea kama sehemu ya mpango wake Rasmi wa Usaidizi wa Maendeleo, ODA.

Jopo la ushauri lililojadili matumizi ya sayansi na teknolojia kwa masuala ya kigeni liliandaa pendekezo na kuliwasilisha kwa waziri wa mambo ya nje Kamikawa Yoko siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita.

Pendekezo hilo linasema sayansi na teknolojia ya hali ya juu ya Japani inapaswa kutumika kikamilifu kwa ODA kutatua matatizo katika nchi zinazoendelea.

Kamikawa alisema hilo litatekelezwa kwanza katika hatua za kukabiliana na mabomu yaliyotegwa ardhini.

Japani ina ujuzi baada ya kushiriki katika miradi ya uondoaji wa mabomu yaliyotegwa ardhini katika nchi kama vile Cambodia.

Wafanyabiashara wa Kijapani hivi karibuni wamekuwa wakitafiti utaratibu huo kwa kutumia teknolojia ya AI na droni. Maafisa wanasema kuna matarajio makubwa kutoka Ukraine na nchi zingine.