Vyombo vya habari: Rais wa Iran na Waziri wa Mambo ya Nje wafariki katika ajali ya helikopta

Vyombo vya habari vya serikali ya Iran leo Jumatatu vimeripoti kwamba Rais Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir Abdollahian na wote waliokuwa ndani ya helikopta iliyoanguka wamefariki dunia.

Jana Jumapili mnamo saa kumi jioni kwa saa za Iran, televisheni ya taifa ya Iran iliripoti kwamba tukio hilo lilitokea katika eneo la mpaka na Azerbaijan.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Ahmad Vahidi alibainisha kuwa ukungu na hali mbaya ya hewa vilisababisha ajali hiyo. Waziri huyo alisema kuwa helikopta hiyo inaonekana ililazimika kutua kwa shida.

Raisi alikuwa akisafiri kutoka kwenye sherehe ya uzinduzi wa bwawa aliyohudhuria pamoja na mwenzake wa Azerbaijan Ilham Aliyev.