Taiwan yajihadhari wakati China ikiongeza shinikizo wakati Lai akiapishwa

Taiwan imemwapisha Lai Ching-te wa Chama ch Democratic Progressive DPP kuwa rais wake mpya leo Jumatatu.

China inamwona Lai kama mtu anayetaka kujitenga, na imekuwa ikiongeza shinikizo lake la kijeshi. Taiwan imekuwa ikifanya maandalizi kwa ajili ya matukio ya dharura yanayoweza kutokea. Imeandaa makazi ya muda kwa wakazi wake endapo litatokea shambulio.

Lai anatarajiwa kudumisha sera ya Rais anayeondoka Tsai Ing-wen ya kutokuwa karibu sana na China.

Tangu kuanza kwa mwezi huu, meli za China zimeingia mara kwa mara kwenye maeneo ya majini ambayo Taiwan inayadhibiti vilivyo. Taiwan inapiga marufuku meli za China kuingia katika maeneo hayo bila ruhusa. Wataalamu wanasema hatua hizo zinalenga kuongeza shinikizo kwa utawala mpya wa Taiwan.