Japani imepitisha mswada wa kutoa adhabu kali zaidi kwa waendesha baiskeli

Wabunge nchini Japani wameidhinisha kwa kauli moja mswada unaotoa adhabu kali zaidi kwa waendesha baiskeli wanaokiuka sheria za trafiki bila kujali.

Marekebisho ya Sheria ya Trafiki Barabarani yalipitishwa na Baraza la Juu la Bunge jana Ijumaa.

Faini ya "tiketi ya bluu" kwa makosa madogo itatumika kwa baiskeli. Mfumo huo tayari unashughulikia magari na pikipiki.

Sheria iliyorekebishwa inataja faini kwa ukiukaji 113 na inatumika kwa watu walio na umri wa miaka 16 au zaidi. Mabadiliko hayo yatatekelezwa ndani ya miaka miwili.

Ajali zinazohusisha waendesha baiskeli zimekuwa zikiongezeka, na polisi wanakabiliana na tabia hatarishi kama vile kupuuza taa za trafiki na alama za kusimama, na matumizi ya simu janja.

Kuendesha baiskeli ukiwa umelewa, ambayo kwa sasa hauna adhabu, kutakuwa na adhabu ya kifungo cha hadi miaka mitatu au faini ya takribani dola 3,200.