Waziri Mkuu wa Japani Kishida alaani upigwaji risasi wa waziri mkuu wa Slovakia

Waziri Mkuu wa Japani Kishida Fumio amelaani shambulio la kupigwa risasi Waziri Mkuu wa Slovak Robert Fico, akilielezea kuwa ni shambulio dhidi ya demokrasia.

Leo Alhamisi, Kishida aliweka ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X -- zamani ukijulikana kama Twitter -- kwamba ameshtushwa sana na habari hiyo na anamwombea Fico apone haraka.

Pia alielezea mshikamano mkubwa kati ya Japani na serikali na watu wa Slovakia.