Vyombo vya habari vya Marekani: Biden aliarifu bunge kuhusu mauzo ya silaha ya dola bilioni 1 kwa Israeli

Vyombo kadhaa vya habari vya Marekani vinasema utawala wa Rais Joe Biden umeliarifu Bunge kuhusu mpango wake wa kuiuzia Israel silaha zenye thamani zaidi ya dola bilioni moja.

Kifurushi hicho kinajumuisha risasi za vifaru na magari ya vita.

Utawala wa Biden ulitangaza wiki iliyopita kwamba ulikuwa unazuia kwa kiasi fulani usambazaji wa silaha kwa Israeli, ili kuonyesha upinzani wake dhidi ya mashambulizi makubwa ya ardhini huko Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Jana Jumatano, Msemajii wa Ikulu ya Marekani Karine Jean-Pierre aliwaambia wanahabari kwamba utawala huo umeelezea wasiwasi juu ya operesheni kubwa huko Rafah.

Lakini aliongeza kuwa kujitolea kwake kwa usalama wa Israel kunabakia kuwa thabiti, na daima umesema utahakikisha kuwa Israel inapata chochote inachohitaji ili kujilinda.

Vyombo vya habari vya Marekani vinasema kuwa uuzaji huo wa silaha unaonyesha hofu ya serikali ya Biden ya kuongeza mgawanyiko wake na Israeli kuhusu Rafah.