Maswali na majibu: Kaa mbali na kazi za muda za udanganyifu (3)

(3) Kupokea na kutuma kifurushi

NHK inajibu maswali kuhusiana na kuhakikisha usalama katika maisha ya kila siku. Kumekuwa na mfululizo wa visa ambavyo wakazi wa kigeni nchini Japani wanajihusisha katika uhalifu baada ya kuomba “kazi rahisi zinazolipa mshahara mkubwa” zinazotangazwa kwenye mitandao ya kijamii. Katika makala hii, tutatoa mifano ya zile zinazoitwa kazi za muda za kutiliwa mashaka ambazo kamwe hupaswi kuzichukua. Katika sehemu ya leo tutaangazia upokeaji na utumaji kifurushi.

Idara ya Polisi ya jiji la Tokyo inaonya dhidi ya matangazo kwenye mitandao ya kijamii ambayo yanaahidi malipo makubwa kwa kile kinachodaiwa kuwa kazi rahisi ya muda ya kupokea vifurushi. Polisi inasema matangazo ya kazi kama hizo hivi karibuni yameonekana kuongezeka kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii yanayotumika na wakazi raia wa kigeni nchini Japani.

Matangazo hayo yanasema kazi inahusisha kutuma kifurushi kilichotumwa nyumbani kwako kukipeleka kwenye anuani iliyochaguliwa, ama kupokea kifurushi katika nyuma maalum ambayo haina wakazi. Idadi inayoongozeka ya watu wanaomba, bila kuhisi kuwa ni uhalifu.

Polisi inasema vifurushi hivyo vinakuwa na vitu kama vile bidhaa zilizonunua kwa njia ya mtandao bila kufuata sheria, kwa kutumia vitambulisho na nywila za watu wengine, fedha zilizopatikana kwa njia ya udanganyifu, na dawa haramu. Wanaonya kuwa kupokea ama kutuma kifurushi kama hicho kunaweza kuwa ni uhalifu. Kwa msisitizo, kupokea kifurushi kunaweza kupelekea shtaka la wizi na makosa mengine. Kuingia katika nyumba isiyokuwa na wakazi ili kupokea kifurushi kunaweza kupelekea kosa lingine la ziada la kuingia bila ruhusa katika sehemu ya mtu.

Polisi inawashauri watu kutojihusisha ikisema kwamba wanaweza kukamatwa kama washirika wa uhalifu mkubwa kwa kile wanachoamini kuwa ni kazi rahisi ya muda.

Taarifa hii ni sahihi hadi kufikia Mei 15, 2024.