Japani yawasilisha malalamiko kwa Korea Kusini baada ya mbunge wake kuzuru Visiwa vya Takeshima

Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Japani Hayashi Yoshimasa anasema amewasilisha malalamiko makali kwa Korea Kusini baada ya mbunge wa upinzani wa nchi hiyo kuzuru Visiwa vya Takeshima katika Bahari ya Japani jana Jumatatu.

Hayashi aliwaambia wanahabari leo Jumanne kuwa ziara hiyo ilifanyika kwa lazima licha ya Japani kuomba mapema ifutwe. Alisema haikubaliki kabisa na ni ya kusikitisha sana kwani visiwa hivyo ni sehemu ya urithi wa Japani, kwa kuzingatia ukweli wa kihistoria na kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.

Korea Kusini inavidhibiti. Japani inadai kuvimiliki na inasema Korea Kusini inavitwaa kinyume cha sheria.