Wapiga kura wa Kashmir kupiga kura katika awamu ya nne ya uchaguzi mkuu wa India

Awamu ya nne kati ya saba za upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa India ilifanyika jana Jumatatu katika maeneo 96 ya uchaguzi kati ya 543 nchini humo.

Usalama uliimarishwa sana huko Srinagar, jiji kuu katika jimbo la Jammu na Kashmir linalodhibitiwa na serikali ya India huku wapiga kura wakielekea katika vituo vya kupigia kura.

Mwaka 2019, serikali ya India ilihitimisha miaka 70 ya uhuru wa jimbo hilo na kuliweka chini ya utawala wake moja kwa moja. Jaribio la serikali la kutaka kuimarisha utawala wake katika eneo hilo kwa kiwango kikubwa halikuungwa mkono katika jimbo hilo lenye Waislamu wengi.

Nadhari inaangazia jinsi wapiga kura wanavyotathmini namna serikali inavyoshughulikia eneo hilo katika uchaguzi mkuu wa kwanza tangu kuhitimishwa kwa uhuru wake.

Wakati wa kampeni za uchaguzi huo, vyama viwili vya kikanda vilitaka uhuru urejeshwe na kumtaka waziri Mkuu Narendra Modi kujiuzulu. Wanachama wa chama kinachoibukia, wakati huo huo, walielezea msimamo wa maafikiano kuelekea sera zake za kiuchumi, ambazo zinaangazia kukuza miundombinu ya utalii na uwekezaji ya eneo hilo.

Kura zote zitahesabiwa mnamo Juni 4.