Putin kumwondoa waziri wa ulinzi Shoigu na kumweka mchumi

Rais wa Urusi Vladimir Putin amempendekeza Waziri wa Ulinzi Sergey Shoigu kuwa katibu wa Baraza la Usalama la Urusi.

Ofisi ya rais wa Urusi imetoa tangazo hilo jana Jumapili.

Putin amekuwa akishughulikia ubadilishaji wa Baraza la Mawaziri tangu alipoapishwa kuanza muhula wake wa tano Mei 7.
Amewasilisha mapendekezo mapya ya uteuzi kwa baraza la juu la bunge.

Shoigu ameongoza wizara ya ulinzi tangu 2012. Nafasi yake itachukuliwa na kaimu Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu Andrei Belousov aliyekuwa mkuu wa sera za uchumi.

Putin pia amempendekeza Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov kubaki katika nafasi hiyo na Mkuu wa Majeshi ya Urusi, Valery Gerasimov naye ataendelea kuwa katika wadhifa huo.

Bado haifahamiki ikiwa baraza jipya lililopendekezwa na Putin linaweza kuleta athari katika vita nchini Ukraine.