Mafuriko yaua watu wasiopungua 160 nchini Afghanistan

Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa ambayo imenyesha katika majimbo ya Kaskazini mwa Afghanistan, yakiwemo Baghlan na Takhar, Ijumaa iliyopita yameua watu wasiopungua 160.

Serikali ya mpito ya Taliban inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia.

Msemaji wa Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Majanga amesema watu zaidi ya 220 wamejeruhiwa katika mafuriko hayo.

Nyumba zaidi ya 8,000 zimeharibiwa kabisa au kiasi na watu wengi wamepoteza makazi yao.

Shirika la Afya Duniani limesema takwimu za hivi karibuni zinaonyesha ongezeko la idadi ya visa vya magonjwa yatokanayo na maji machafu kama kuharisha na maambukizi ya ngozi kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko.