Waandamanaji wakusanyika kupinga muswada wa ushawishi wa kigeni nchini Georgia

Umati mkubwa wa watu umekusanyika katika mji mkuu wa Georgia Tbilisi, kupinga muswada ambao wanasema unalenga kudhibiti taasisi ambazo zinapokea fedha za mataifa ya kigeni.

Muswada huo ulitambulishwa na chama tawala. Ikiwa utapitishwa, bunge litahitaji taasisi zisizokuwa za kiserikali na vyombo vya habari vinavyopokea asilimia zaidi ya 20 ya fedha zao kutoka nje ya nchi kuandikisha kama mawakala wa ushawishi wa kigeni.

Waandamanaji wanasema kwamba muswada huo ni sawa na sheria ya Urusi ambayo ilitumiwa na serikali kupunguza shughuli za taasisi na vyombo vya habari ambavyo serikali inaona si rafiki.

Huku upigaji kura wa muswada huo ukitarajiwa kufanyika hivi karibuni, makumi ya maelfu ya watu waliandamana katika uwanja mmoja uliopo katikati mwa Tbilisi jana Jumamosi.

Washiriki walisema kwamba Georgia iliyo huru na yenye demokrasia haihitaji muswada wa aina hii.

Mshiriki mmoja alisema kwamba kiuhalisia ni sheria ya Urusi ambayo itakuwa kikwazo kwa matumaini ya Georgia kujiunga na Umoja wa Ulaya, akielezea matumaini kwamba maandamano yatasaidia kufanya muswada huo ukataliwe.

Mshiriki mwingine alisema kwamba wanahitaji kupinga kwa ajili ya mustakabali wao.

Georgia imeomba kujiunga EU lakini chama tawala kilichoanzisha taifa hilo kinasemekana kuwa karibu na Urusi.

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alisema kwenye mitandao ya kijamii kuwa “Wito wa raia wa Georgia kwa demokrasia ya huru na jamii anuai lazima uzingatiwe.