Mafuriko yaua watu wasiopungua 85 nchini Afghanistan

Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizolikumba jimbo la Baghlan lililopo kaskazini mwa Afghanistan siku ya Alhamisi na Ijumaa yameua watu wasiopungua 85.

Picha za video zilizopigwa juzi Ijumaa zinaonesha maji ya matope yakielekea kwenye maeneo ya makazi na yakiyakumba majengo.

Mamlaka za eneo hilo zilizopo chini ya utawala wa muda wa serikali ya Taliban zilisema mamia ya majengo yaliharibiwa ama kusombwa na maji.

Maafisa wa serikali na maeneo wametoa timu za uokozi ili kutafuta watu ambao hawajulikani mahali walipo.

Mvua kubwa ambazo zimeikumba nchi hiyo mwezi uliopita ziliua watu wasiopungua 70 na kuharibu majengo zaidi ya 2,000.