Familia za waliotekwa zatoa tena wito kwa Japani na Korea Kaskazini kulitatua suala hilo

Familia za raia wa Japani waliotekwa nyara na Korea Kaskazini zimetoa tena wito wao wa kutatuliwa kwa suala hilo ili wazazi wanaozeeka waweze kuungana tena na watoto wao.

Kikundi cha familia hizo na watu wanaowaunga mkono kilifanya mkutano wa hadhara jijini Tokyo jana Jumamosi. Takribani watu 800 walishiriki tukio hilo, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Kishida Fumio.

Kiongozi wa kikundi hicho Yokota Takuya alisema Arimoto Akihiro mwenye umri wa miaka 95, baba wa Arimoto Keiko, na mama yake Sakie mwenye umri wa miaka 88 ndio wazazi pekee waliohai wa waathirika.

Dada yake mkubwa Megumi alitekwa mwaka 1977 pale alipokuwa na umri wa miaka 13.

Aliliita suala la mateka kuwa ni la haki za kibinadamu na suala kibinadamu lenye muda mdogo.

Aliishauri serikali kuendelea kufanya majadiliano bila kuweka masharti magumu ambapo waathirika wote watarejea mara moja.

Yokota Sakie alisema familia yake imekuwa ikimsubiri Megumi arejee bila kujua wapi alipo. Alitoa wito kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kubadili mawazo yake na kuwarejesha mateka wote kwa wazazi wao.

Mwathirika wa zamani wa kutekwa nyara Soga Hitomi ambaye alirejea Japani miaka 22 iliyopita, pia alizungumza katika mkutano huo wa hadhara. Mama yake Miyoshi alitekwa pamoja na yeye mwaka 1978 na bado hajulikani mahali alipo.

Soga alisema leo Jumapili ni Siku ya Mama nchini Japani lakini ameshindwa kusherehekea siku hiyo kwa miaka 46, akiongeza kuwa hawezi kuelewa kwanini yeye na mama yake wanapaswa kupitia hatma hiyo.

Pia alisema muda unazidi kwenda na anatumai kwamba mateka wote watarejea nyumbani mapema iwezekanavyo.

Washiriki wa mkutano huo wa hadhara walitoa azimio ambalo linatoa wito kwa serikali kuwarejesha mateka wote nyumbani kwa pamoja mara moja na Korea Kaskazini kuamua kuwarejesha makwao waathirika.