Kishida aapa kufanyia kazi suala la mateka katika mkutano na Kim Jong Un

Waziri Mkuu wa Japani Kishida Fumio ameahidi kuongeza juhudi za kufanya mkutano na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ili kuwarejesha raia wote wa Japani waliotekwa na Korea Kaskazini.

Akizungumza katika maadamano yaliyoandaliwa na ndugu wa mateka hao jana Jumamosi jijini Tokyo, Kishida alisema suala la mateka ni dharura ya kibinadamu lenye muda mdogo, kwa kuwa ndugu wengi umri unakwenda.

Alisema serikali itafanya kila itakavyoweza kuwarejesha nyumbani mateka hao mapema iwezekanavyo.

Kishida alisisitiza umuhimu wa mabadiliko ya haraka katika suala hilo. Aliongeza kuwa ni muhimu kwa viongozi wakuu kuunda uhusiano ambao utawawezesha kuzungumza kwa uwazi ili kutatua masuala magumu.

Alisema anadhamiria kukutana na Kim muda wowote bila masharti.

Waziri mkuu huyo wa Japani pia alisema ataongeza juhudi kupitia njia mbalimbali ili kuendeleza mazungumzo ya ngazi ya hali ya juu chini ya maelekezo yake moja kwa moja ili kufanikisha mkutano huo wa viongozi wakuu.

Kishida aliongeza kuwa anataka kumshauri Kiongozi wa Korea Kaskazini kuona taswira kubwa, kuondokana na vikwazo na kufanya maamuzi pamoja.