Ukraine: Wanajeshi wa Urusi katika eneo la Kharkiv wanalenga kuunda eneo la kinga kwenye mpaka

Jeshi la Ukraine linasema kuwa wanajeshi wa Urusi wamevuka mpaka na kuingia katika eneo la mashariki la Kharkiv, na kuna uwezekano mkubwa wa kuanzisha eneo la kinga kati ya nchi hizo mbili.

Gavana wa Kharkiv alisema kwenye mitandao ya kijamii jana Ijumaa kwamba Warusi wameanza hatua mpya ya mashambulizi kaskazini mwa Kharkiv.

Gavana huyo alisema eneo lililo karibu na mpaka na Urusi lilikumbwa na mashambulizi makali na raia wawili kuuawa.

Afisa wa Mnadhimu Mkuu wa jeshi la Ukraine aliiambia NHK kwamba wanajeshi wa Urusi wameingia kutoka kaskazini, na kusonga mbele kilomita moja katika eneo hilo.
eo hilo.