Biden: Marekani haitaipatia Israel silaha iwapo itafanya mashambulizi Rafah

Rais wa Marekani Joe Biden anasema atasitisha kusafirisha silaha za Marekani kwenda Israel iwapo vikosi vya Israel vitafanya mashambulizi ya ardhini huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Biden alitoa maoni hayo kwenye mahojiano na CNN jana Jumatano.

Hii ni mara ya kwanza kwa Biden kuzungumza hadharani kuhusu kusitisha usambazaji wa silaha kwa Israel tangu vita kati ya Israel na Hamas ilipoanza mwezi Oktoba mwaka jana.
###